Jumatano 14 Mei 2025 - 10:38
Muqtada Sadr akutana na Ayatollah al-Udhma Jawadi Amoli katika mji mtukufu wa Najaf

Hawza/ Kiongozi wa harakati ya Sadr amemtembelea Ayatollah Abdullah Jawadi Amoli sehemu aliyo fikia huko mjini Najaf al-Ashraf na kufanya naye mazungumzo.

Kwa mujibu wa idara ya tarjama ya Shirika la Habari la Hawza, ikinukuu kutoka katika shirika la habari la "Ninai" la Iraq, Moqtada Sadr, kiongozi wa harakati ya Sadr nchini Iraq, amekutana na Ayatollah Abdullah Jawadi Amoli, miongoni mwa wanazuoni wakubwa wa Iran, sehemu aliyo fikia Ayatollah huyo huki mjini Najaf al-Ashraf.

Ofisi maalumu ya Hujjatul-Islam wal-Muslimin Sadr imetangaza kuwa yeye, sambamba na kumkaribisha Ayatollah Jawadi Amoli kama mgeni mashuhuri katika mji wa Amirul-Mu’minin (as), alimtakia afya njema, kukubaliwa kwa ibada zake, na ukaaji wenye furaha.

Kwa upande mwingine, Ayatollah Jawadi Amoli naye alielezea furaha na shukrani zake za dhati kwa ziara hiyo.

Inaelezwa kuwa, Ayatollah Jawadi Amoli katika ziara yake ya kuelekea kwenye maeneo matukufu ya Kiislamu, amefanya mikutano mbalimbali na maulamaa wakubwa wa Hawza ya Najaf, wakiwemo marjaa wa daraja ya juu kabisa, Ayatollah al-Udhma Sistani, jambo linalodhihirisha umuhimu wa uhusiano wa kielimu na kimaanawi kati ya vituo vya Kishia katika nchi hizi mbili.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha